Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:00

Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania wakaribishwa kuwekeza Sudan Kusini


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (L), na kiongoiz wa Upinzani Riek Machar wakiwa katika hafla ya kusaini makubaliano ya amani Ikulu ya Ju Juba, April 3, 2022.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (L), na kiongoiz wa Upinzani Riek Machar wakiwa katika hafla ya kusaini makubaliano ya amani Ikulu ya Ju Juba, April 3, 2022.

Serikali ya  Sudan Kusini imewasihi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania kutumia fursa ya kuangalia maeneo mbali mbali na sekta za madini, mafuta au kilimo na kufikiria ni katika sekta gani wanataka kuwekeza katika taifa hilo changa duniani.

Hayo yalisemwa na naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudan Kusini, Agok Makur, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kibiashara kati ya Tanzania na Sudan KUsini uliofanyika mjini Juba.

Ujumbe wa wawekezaji 50 na wamiliki wa biashara kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaitembelea Juba wiki hii kuangalia fursa za biashara nchini Sudan Kusini wakati wakihudhuria mkutano wa siku tatu ulioanza Jumatano.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Makur anawasihi wamiliki wa biashara nchini Tanzania kutembelea maeneo mbalimbali nchini humo na sekta nyingine kama vile za madini na mafuta.

“Sisi kama serikali ya Sudan Kusini, tunawakaribisha wafanyabiashara wote kuja na kuwekeza Sudan Kusini kwa sababu tuna rasilmali nyingi nchini Sudan Kusini ikitoa fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuja humu nchini, baada ya kusaini mkataba wa amani Sudan Kusini, sisi kama serikali ya umoja wa kitaifa tunafanya kazi kukabiliana na hali ya uchumi wa Sudan Kusini.

Sehemu ya machimbo ya mafuta nchini Sudan Kusini, January 21, 2019. Picture taken January 21, 2019. REUTERS/Samir Bol - RC150EBBFA70
Sehemu ya machimbo ya mafuta nchini Sudan Kusini, January 21, 2019. Picture taken January 21, 2019. REUTERS/Samir Bol - RC150EBBFA70

Yel Koor, Waziri Mdogo wa Wizara ya Uwekezaji ya Sudan Kusini anasema kuna fursa nyingi kwa wawekezaji kutoka nje.

“Kituo cha kipaumbele cha uwekezaji kimewekwa na serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, ikijumuisha sekta ya kilimo, sekta ya miundombinu, sekta ya madini, sekta ya nishati na sekta ya utalii na sekta za kijamii, elimu na afya, na wawekezaji katika sekta hizi wanahaki kwa maslahi na motisha zilizopo.”

Ulingeta Mbamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, anasema ujumbe wa biashara unawasaidia wamiliki wa biashara Tanzania kufikia masoko ya Sudan Kusini.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Sudan Kusini ni moja ya nchi za Afrika Mashariki, lakini kwa bahati mbaya kutokana na hali ya kijiografia halifanyi vizuri kibiashara na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuliona itakuwa vyema kuja hapa, kuzungumza na marafiki zetu na kujadili kidogo, kwa sababu bado tunafikiria ni muhimu kufanya biashara ya ndani kabla hatujafikiria kufanya biashara na nchi za Ulaya, Marekani na China.”

Mbamba says there are already a few Tanzanian businesses in Juba but the level of investment remains low compared to what Tanzania is doing in other East African countries like Kenya, Uganda, Rwanda, and Burundi.

Mbamba anasema tayari kuna wafanyabiashara watanzania wachache mjini Juba lakini kiwango cha uwekezaji bado kiko chini ukilinganisha na biashara ambayo Tanzania inafanya na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Ujumbe wa Tanzania utakutana na maafisa wengine mbalimbali wa serikali ya Sudan Kusini kutoka wizara za barabara na madaraja, mawasiliano na ICT, afya, mafuta na madini.

Ripoti hii ni ya mwandishi wa VOA Juliana Siapai, Juba, Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG