Asilimia hiyo ya watu waliojitokeza katika duru ya kwanza ya mwezi Desemba, wakosoaji wa rais walisema inadumaza madai yake ya kuungwa mkono na umma kwa mabadiliko makubwa ya kisiasa.
Huku vyama vya siasa vikisusia upigaji kura, wagombea wengi ni huru na huenda watu wakaangazia kama kutakuwa na ushiriki mkubwa kuliko ilivyokuwa Desemba.
Tume ya uchaguzi ilisema kwamba waliojitokeza walikuwa asilimia 4.7 mpaka ilipofika saa tano asubuhi siku ya Jumapili, saa tatu baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa. Mwezi Desemba ilitangazwa kuwa waliojitokeza ilikuwa ni kiasi cha asilimia 3 ilipofika saa 4 asubuhi.
Tume hiyo itatumia takwimu za leo Jumapili kama ya jumla ya idadi kwa duru zote mbili za uchaguzi na upinzani umesema unahofia mamlaka itajaribu kubadili takwimu kwa kuongeza idadi.