Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 00:47

Wabunge wakataa kuunga mkono kuendeleza hali ya dharura mashariki mwa DRC

Wabunge wakiwa nje ya bunge mjini Kinshasa, baada ya polisi kufunga milango yote.Juni 12,2020. (Twitter/Bunge la DRC)
Wabunge wakiwa nje ya bunge mjini Kinshasa, baada ya polisi kufunga milango yote.Juni 12,2020. (Twitter/Bunge la DRC)

Wabunge wa mashariki ya jamhuri ya Congo wameonya kuongezeka mauwaji katika eneo lao na kusema kwamba takriban raia 144 wameuawa mwezi huu, wabunge hao wamekataa pia kuunga mkono kuendeleza hali ya dharura ambayo walisema inafeli dhamira yake ya kumaliza miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu.

Licha ya pingamizi la wabunge hao, bunge siku ya Jumatano liliidhinisha hoja ya kuongeza miuda wa hali ya dharura kama inavyofanyika kila baada ya wiki mbili.

Chini ya mpango wa dharura serikali mwezi Mei ilibadilisha tawala za kiraia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri na kuweka maafisa wa polisi na wanajeshi, lakini ripoti ya bunge mwezi uliopita ilikosoa ukosefu wa mipango na ufadhili sahihi.

Raia wameuawa kwa kiwango sawa na kabla ya hali ya dharura kwa mujibu wa data kutoka Kivu Security Tracker, ambayo inaweka ramani ya ghasia katika eneo ambalo zaidi ya makundi 120 ya waasi yanaendesha shughuli zake.

Tumegundua kwa masikitiko kwamba serikali haijaweka hatua yoyote madhubuti au ishara kali ambayo inaweza kukidhi wasiwasi wetu," wabunge 48 kutoka mashariki walisema katika tamko la pamoja.

XS
SM
MD
LG