Kanali Mamady Doumbouya kiongozi wa utawala wa kijeshi aliyechukua madaraka kwa njia ya mapinduzi Septemba mwaka 2021, amesema mwezi huu, kuwa inaweza kuchukua zaidi ya miaka mitatu kwa taifa hilo la Afrika Magharibi kurejea katika utawala wa kiraia.
Ameiambia televisheni ya taifa baada ya mashauriano ya kisiasa kuwa alikuwa akizingatia kipindi cha mpito cha miezi 39, hii ikiwa ni mara ya kwanza kupendekeza ratiba hiyo.
Vyama vikuu vya kisiasa na zaidi ya washirika wake vyama vidogo 60 katika taarifa yao ya pamoja wametupilia mbali mapendekezo hayo na kuomba viongozi wa mpito kutetea taasisi za kidemokrasia.
Wamesema baraza linalojulikana kama NTC, lilioundwa na Junta kufanya kazi kama bunge hadi pale uchaguzi utakapofanyika, bado halijapitisha ratiba na wametoa wito kufanyika majadiliano na pande zote husika ikiwemo jumuiya za kiraia.