Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:13

Baadhi ya vyama vya Siasa Nchini DRC havitaki Mjadala wa Kisiasa


Kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi (mbele), rais wa chama cha upinzani cha UDPS , anahudhuria mkutano wa 14 wa nchi zinazozunguma kifaransa mjini Kinshasa mwezi Oktoba.
Kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi (mbele), rais wa chama cha upinzani cha UDPS , anahudhuria mkutano wa 14 wa nchi zinazozunguma kifaransa mjini Kinshasa mwezi Oktoba.

Chama kikuu cha upinzani nchini DRC cha UDPS, hakionekana kutoa waraka wowote kwa umma kujibu wito wa rais wa kuitishwa mjadala kwa kisiasa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:35 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Lakini msemaji wa UDPS, Augustin Kabuya kuwa bila ya hivyo uchaguzi hauwezi kufanyika.

Anasema hatuwezi kuongoza watu kwenda kwenye vituo vya kura ambavyo vitakuwa na kasoro kuanzia mwanzo. Kila mtu anafahamu, anasema , kwamba hakuna matayarisho yaliyofanywa kwa ajili ya mzunguko wa uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika mwaka 2016, na licha ya baadhi ya watu kusema twendeni tukapige kura.

Kabuya amepinga shutuma kwamba chama chake kina mipango ya kufikia makubaliano ya kushirikiana madaraka na rais Kabila, ili kumruhusu abakie mamlakani baada ya kipindi chake kikatiba kufikia hatima yake ya kuongoza kwa mihula miwili, kipidni ambacho mwisho wake ni Disemba mwaka ujao.

Amesisitiza kwamba kiongozi wa chama chake, Etienne Tshisekedi, alikuwa mshindi wa kweli wa uchaguzi wa rais wa mwaka 2011, ambapo rasmi alishika nafasi ya pili na kwamba hivyo ni haki kwa UDPS kufanya mashauriano na Kabila.

Kabuya anasema chama chake kinataka uchaguzi ufanyike kwa wakati, ndani ya kipindi cha kumalizika muhula wa pili wa uongozi wa bwana Kabila lakini kwa hilo kuweza kutokea wanahitaji kukaa chini na kujadili masuala ya uchaguzi.
makundi mengine mawili ya upinzani yanayojulikana kama G7 na Opposition Dynamic wametaka wiki hii na kutoa taarifa ya pamoja iliyosomwa na Ingele Ifoto wa Opposition Dynamic.

Taarifa imesema ajenda ya kabila kwa mjadala, ambapo inajumuisha majadiliano ya mabaidliko ya mfumo ya uchaguzi, ni dhahiri inaonyesha kuwa ana azma ya kubakia madarakani. Pia imeishutumu serikali yake kwa kushindwa katika mambo mengi.

Rais amesema makundi ya kijamii yatakaribishwa katika mjadala. Mwanachama wa kundi la kutetea haki la ASADHO, jean Claude Katende ameiambia VOA kwamba ajenda ya kabila ya kuitisha mjadala imezidi kuongeza wasi wasi kwamba anafikiria kubadili katiba. Amesema ajenda imelenga katika kuitisha uchaguzi wa rais usio wa moja kwa moja.

Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema rais ana azma ya kuheshimu katiba.

XS
SM
MD
LG