Vurugu za kijamii zinazohusishwa na hisia za kidini zimeenea mjini Dar es Salaam na kisiwani Unguja Ijumaa huku hali ikiwa shwari mjini Mombasa, Kenya, ambako nako vurugu za kijamii na kisiasa zimekuwa zikiendelea kwa wiki nzima sasa.
Mjini Dar es Salaam polisi na askari wa kuzuia fujo walienezwa kwa wingi katika maeneo kadha ya mji huo kudhibiti vurugu zilizotazamiwa baada ya sala ya Ijumaa ambapo wafuasi wa kiongozi wa kundi moja la kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda wanadai kiongozi huyo aachiliwe baada ya kukamatwa na polisi mapema wiki hii.
Viongozi kadha wa kiislamu na maafisa wa serikali walitoa wito kwa wananchi kutoshiriki katika machafuko yoyote, laki ni rai hizo hakizusikilizwa kwa makini. Watu kadha walienea katika maeneo mengi mjini kama vile Kariakor na Magomeni lakini polisi, wanajeshi na askari wa kuzuia fujo ulifanikiwa kuzuia ghasia kutokea kwa kujieneza mitaani na kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu. Watu kadha wametiwa nguvuni.
Huko Zanzibar nako polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao kwa muda wa wiki nzima hii wamekuwa wakitaka kujua alipo kiongozi wa kundi la Uamsho, Sheikh Farid, ambaye inadaiwa alitoroshwa mapema wiki hii.
Shughuli za biashara zimesimama mjini Zanzibar, watoto wameshindwa kwenda shule kutokana na vurugu zinazoendelea tangu Sheikh Farid atoweke