Viongozi wa Qatar na Kuwait wamepokea mwaliko Jumatatu kwa mkutano wa viongozi mjini Cairo utakaofanyika Jumamosi ili “kujadili maendeleo na mustakbali wa Palestina na mchakato wa amani".
Vyombo vya habari vya serikali katika nchi zote mbili vilitangaza mualiko huo siku moja baada ya Cairo kutangaza nia yake ya kuandaa “mkutano wa kikanda na kimataifa kuhusu mustakbali wa Palestina”, wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.
Baraza la Ushirikiano wa Ghuba pia lilitangaza Jumatatu litafanya mkutano wa kipekee wa mawaziri wake wa mambo ya nje Jumanne, “kujadili maendeleo ya hali katika Ukanda wa Gaza”.
Siku kumi baada ya vita vilivyozuka kati ya Hamas na Israel, juhudi za kidiplomasia zimeleta mafanikio kidogo, wakati viongozi wa kikanda na wa dunia wakijaribu kupata misaada ya kibinadamu na kuzuia umwagikaji damu wowote kusambaa.
Forum