Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:10

Viongozi wa Afrika wameyataka makundi yenye silaha DRC yaondoke maeneo wanayoyakalia kimabavu


Viongozi katika mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia
Viongozi katika mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia

Wakuu wa nchi "walielekeza kuondolewa kwa makundi yote yenye silaha ifikapo tarehe 30 Machi 2023 kutoka maeneo yanayokaliwa kimabavu", Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema kwenye Twitter baada ya mkutano mdogo wa kilele mjini Addis Ababa

Viongozi wa Afrika wametoa wito siku ya Ijumaa kwa makundi yote yenye silaha kujiondoa katika maeneo yanayokaliwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao, jumuiya ya kikanda ya EAC imesema.

Wakuu wa nchi "walielekeza kuondolewa kwa makundi yote yenye silaha ifikapo tarehe 30 Machi 2023 kutoka maeneo yanayokaliwa kimabavu", Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema kwenye Twitter baada ya mkutano mdogo wa kilele mjini Addis Ababa.

Pia wamependekeza "kusitishwa mara moja kwa mapigano" na makundi yote yenye silaha na watu waliokoseshwa makazi yao kutokana na ghasia zilizotokea mashariki mwa nchi hiyo kupatiwa makazi, iliongeza. Mkutano wa nchi saba za EAC ulifanyika kwenye mkesha wa kuamkia Jumamosi katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaofanyika jumamosi katika mji mkuu wa Ethiopia.

XS
SM
MD
LG