Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari kwamba shirika la Umoja wa Mataifa linachunguza pamoja na wadhibiti wa India na mtengenezaji wa dawa, Maiden Pharmaceuticals yenye makao yake mjini New Delhi.
Maiden Ilikataa kutoa maoni yake kuhusu tahadhari hiyo, huku simu na ujumbe wa maandishi wa Reuters kwa Mdhibiti Mkuu wa Dawa nchini India zikiita bila kujibiwa. Gambia na wizara ya afya ya India pia hazikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.
WHO pia ilitoa tahadhari ya bidhaa za matibabu ikiwataka wadhibiti kuondoa bidhaa za Maiden Pharmaceuticals kwenye masoko.