Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:28

Uturuki inawashikilia watu 67 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na PKK


Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Yerlikaya akizungumza na waandishi wa habari
Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Yerlikaya akizungumza na waandishi wa habari

Msako huo unawalenga wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) umekuja siku chache baada ya kundi hilo kudai kuhusika na shambulio la bomu la kujitoa mhanga mjini Ankara ambalo liliwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

Uturuki imesema Jumanne kuwa inawashikilia takriban watu 67 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo wa Kikurdi.

Waziri wa mambo ya ndani, Yerlikaya amesema mamlaka zilifanya uvamizi katika majimbo 16. Msako huo unawalenga wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) umekuja siku chache baada ya kundi hilo kudai kuhusika na shambulio la bomu la kujitoa mhanga mjini Ankara ambalo liliwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

Uturuki ilifanya mashambulizi ya anga saa chache baadaye dhidi ya maeneo ya PKK kaskazini mwa Iraq mahala ambako kundi hilo lina makao yake. Kundi la PKK ambalo linatajwa kuwa kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya limekuwa likiendesha uasi wa miongo kadhaa nchini Uturuki.

Forum

XS
SM
MD
LG