Maafisa wa afya wanajaribu kufanya utafiti kujua nani katika ndege kadhaa kote Afrika Magharibi wiki iliyopita alikuwa karibu na mtu mmoja ambaye baadae alikufa kwa ugonjwa wa ebola.
Patrick Sawyer alipanda ndege huko Liberia, iliyopitia Ghana na kubadilisha ndege nchini Togo kuelekea Nigeria ambako alikufa kutokana na virusi vya ebola ijumaa iliyopita.
Sawyer aliwekwa katika chumba cha pekee mara alipowasili Nigeria lakini abiria wengine waliruhusiwa kuondoka katika uwanja wa ndege mara walipogundua kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo.
Mashahidi wanasema Sawyer alikuwa anatapika na kuharisha katika moja ya ndege alizopanda.
Lakini wataalamu wa afya wanasema hiyo haitoshi kuambukiza wengine. Ili kuambukizwa ebola inahitaji mgusano wa majimaji na mtu aliyeathiriwa.