Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:14

Ushindani mkubwa kati ya Odinga na Kenyatta


Mgombea urais na Waziri Mkuu aliyepo madarakani Raila Odinga
Mgombea urais na Waziri Mkuu aliyepo madarakani Raila Odinga
Matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika karibuni katika uchaguzi wa urais Kenya yanaonyesha Waziri Mkuu Raila Odinga anapambana vikali na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, ikiwa imebaki wiki moja tu kabla ya upigaji kura kufanyika.

Katika kipindi cha wiki tatu zilizopita Odinga amekuwa akitoa hotuba ya aina hiyo hiyo katika kila mikutano yake ya kampeni kote nchini humo. Anaahidi elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, kuboresha njia za huduma za afya na kuongeza fedha kwa vijana wajasiliamali. Anauambia umati wa wapiga kura kwamba kuimarisha program za jamii za wakenya kutaboresha uchumi wa nchi.

Bwana Odinga anasema anapanga kuendelea na pointi hizo hizo alizozitoa katika kampeni zilizopita hata kama kura za maoni za karibuni zinaonyesha amepoteza kuwa mbele na sasa yuko sambamba na Uhuru Kenyatta.

Kura za maoni zinampa Naibu Waziri Mkuu Kenyatta ushindi katika mdahalo wa kwanza kuwahi kufanyika nchini humo wa mwanzoni mwa mwezi huu. Wakati Odinga akisisitiza program zake za kijamii, wagombea urais saba wengine wana sera zinazolingana.

Kila mgombea anaahidi kutoa elimu bure ya msingi na sekondari. Bwana Kenyatta pia anaahidi kutoa bure huduma za afya, japokuwa ataelekeza kwanza kwenye makundi kama vile wanawake wajawazito na wagonjwa wa HIV.

Na kati ya wagombea wawili wanao-ongoza, mustakbali wa sera za bwana Kenyatta unatoa maelezo ya kina ya program za kuwahamasisha vijana na ubunifu wa ajira, suala kuu hivi sasa pamoja na ongezeko la vijana wasio na ajira nchini humo.
XS
SM
MD
LG