Upinzani nchini Zimbabwe umesema Jumapili utapinga matokeo ya uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ambao unaweza kukipa chama tawala wingi wa kutosha kubadilisha katiba.
Taifa hilo la Afrika Kusini lilitarajiwa kufanya uchaguzi mdogo wa majimbo tisa siku ya Jumamosi, lakini wagombea wengi wa upinzani waliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura na mahakama, katika kipindi cha ghasia za uchaguzi.
Chama cha Rais Emmerson Mnangagwa, cha ZANU-PF, kinaangazia viti 10 kuelekea kupata wingi wa theluthi mbili ya viti bungeni ambavyo vitaiwezesha kubadilisha katiba.
Uchaguzi mdogo uliofanyika ni udanganyifu, chama kikuu cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC), kilisema katika taarifa yake siku ya Jumapili, kikielezea kama mapinduzi ya mahakama, na ukweli usiopingika dhidi ya katiba ya Zimbabwe.
"Kulingana na sheria, tutawasilisha malalamiko rasmi kwa tume ya huduma za mahakama", ilisema taarifa ya chama hicho.
Forum