Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

UN yaelezea hali ya haki za kibinadamu Jamhuri ya Afrika ya Kati


Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.
Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk alisema watoto hawalindwi na migogoro ambayo imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2012 akielezea hasa wasichana wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kutisha vya ukatili wa ngono vinavyohusishwa na migogoro hiyo

Tathmini iliyofanywa na wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati inaonyesha kwamba ghasia za kikabila zilizokithiri na ukiukwaji mkubwa wa kimfumo kote nchini humo huku watoto wakikabiliwa na unyanyasaji na ukatili wa kutisha mikononi mwa makundi yenye silaha, vikosi vya ulinzi na usalama, na makampuni binafsi ya kijeshi na usalama.

Ni nadra sana kuikuta nchi yenye rekodi ya haki za binadamu ambayo inatisha sana imesahaulika na mataifa mengine duniani amesema Volker Türk, kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ufunguzi wa taarifa yake kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.

Alisema watoto hawalindwi na migogoro ambayo imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2012 akielezea hasa wasichana wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kutisha vya ukatili wa ngono vinavyohusishwa na migogoro hiyo.

Ripoti zilizopokelewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zinakadiria kuwa makundi yenye silaha yaliyotia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2022 yalihusika kwa asilimia 35 ya ukiukaji uliorekodiwa, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara, kuwekwa kizuizini, kutendewa vibaya, uharibifu wa miundombinu na uidhinishaji wa mali.

XS
SM
MD
LG