Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:44

UN yaadhimisha miaka 75 wakati ushirikiano wa kimataifa unadhoofika


Mkutano wa kuadhimisha miaka 75 ya Umoja wa Mataifa
Mkutano wa kuadhimisha miaka 75 ya Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asikitishwa na ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hi leo, alipokuwa anafungua mkutano wa viongozi kuadhimisha miaka 75 tangu kuundwa kwa umoja huo.

Akizungumza kutokea ukumbi mkuu wa umoja huo mjini New York Jumatatu kabla ya viongozi wa duania kuanza kutoa hotuba zao za kila mwaka kupitia mtandaoni, Guterres amesema "hakuna anayetaka serikali moja ya dunia nzima lakini, ni lazima kufanyakazi kwa pamoja ili kuimarisha utawala bora."

Umoja wa Mataifa unaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake bila ya shamra shamra, mikutano na matukio mbalimbali kama ilivyokuwa kawaida kutokana na janga na virusi via corona.

Kila nchi itawakilishwa na mwanadiplomasia mmoja kutoka kwenye ubalozi wao mjini New York kwenye mkutano huo utakaofanyika kupitia mtandaoni.

Uwanja nje ya Umoja wa Mataifa ukiwa mtupu wakati wa kuadhimisha miaka 75
Uwanja nje ya Umoja wa Mataifa ukiwa mtupu wakati wa kuadhimisha miaka 75

Sherehe hizo zilizotarajiwa kuanzisha mkutano huo, ambao kwa kawaida huwaleta pamoja viongozi kutoka karibu mataifa 200 ya dunia pamoja na mawaziri mabalozi, waandishi wa habari na wanaharakati wa masuala mbalimbali.

Mkutano wa viongozi mwaka 2020 unafanyika katikati ya janga na Covid-19 na kuzusha hoja mpya juu ya ushirikianio wa kiamtaifa. Karibu viongozi 180 wamealikwa kutoa hotuba ya dakika tatu tu kupitia video, pale mkutano wa Baraza Kuu utakapoanza Jumanne.

Rais Trump ataufungua rasmi mkutano huo mkuu Jumanne, wakati utawala wake ukitangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran, ukieleza kwamba vimekubaliwa na Umoja wa Mataifa lakini takriban mataifa yote ya dunia yanapinga jambo hilo.

Katibu Mkuu Guterres amesema, "nina sikitishwa kwamba tunapoteza nafasi nyeti kwa viongozi kukutana kwani ili diplomasia kufanikiwa kunahitaji watu kukutana pamoja."

Wachambuzi wanasema nchi nyingi zimelazimika kuchukua hatua za kibinafsi kutokana na janga la Covid-19, baada ya mipaka kufungwa na ushirikiano kupungua.

Mbali na hotuba kwenye mkutano mkuu kutakuwepo na mikutano mengine juu ya masuala muhimu ya dunia, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, migogoro ya dunia ikiwa ni Libya na Lebanon, hali ya uchumi na ukosefu wa ajira.

XS
SM
MD
LG