Matamshi yake yamekuja wakati kiongozi wa utawala huo wa Taliban Hibatullah Akhun-dzada akisisitiza wito wake wa kufikia malengo ya kufanya marekebisho ya kidini kwenye jamii ya Afghanistan, kupitia usimikaji wa sheria kali za kiislamu au Sharia. Mohammed ameyasema hayo wakati wa hotuba yake kwenye chuo cha masuala ya umma na kimataifa cha Princeton, jimboni New Jersey, akisema kwamba kongamano lao litaleta pamoja wajumbe kwa ajili ya Afghanistan kutoka kote ulimwenguni kwenye meza ya mazungumzo , miongoni mwa masuala mengine. Ameongeza kusema kwamba hilo huenda likafanyika katika wiki mbili zijazo kwenye eneo hilo, kwa mara ya kwanza likiwaleta pamoja wajumbe wa kieneo na kimataifa, pamoja na katibu mkuu wa UN.
VOA Direct Packages
UN kushinikiza kutambuliwa kwa utawala wa Taliban wa Afghanistan
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed Jumatatu amesema kwamba Umoja huo anapanga kongamano katika siku zijazo ili kujadili kutambuliwa kwa utawala wa Taliban wa Afghanistan, akisisitiza uhumhimu wa kushirikiana na utawala huo.