Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 23:38

Ukraine itakuwa ikituma boti zilizojaa mbegu barani Afrika-Kuleba


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alipohudhuria Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Ny.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alipohudhuria Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Ny.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, aliahidi kuwa nchi yake iliyoko vitani  itafanya kila iwezalo kupeleka nafaka zaidi barani Afrika alipokuwa akianza ziara yake wiki hii katika bara hilo nchini Senegal.

Ukraine itakuwa ikituma boti zilizojaa mbegu barani Afrika, Kuleba alisema baada ya kukutana na rais wa Senegal na waziri wa mambo ya nje mjini Dakar siku ya Jumatatu.

"Tutafanya tuwezavyo hadi pumzi ya mwisho kuendelea kusafirisha nafaka ya Ukraine barani Afrika na duniani kote kwa ajili ya usalama wa chakula," Kuleba alisema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Senegal, Aissata Tall Sall.

Rais wa Senegal Macky Sall, mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, amezitaka Russia na Ukraine kurejesha mauzo yao ya nafaka nje ya nchi licha ya vita vinavyoendelea.

XS
SM
MD
LG