Akizungumza na wanahabari akiwa na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borell, Kuleba amesema kwamba Ukraine imekuwa kwenye majadiliano mazito na wabunge wa Marekani wa vyama vya Demokrat na Repablikan.
Ameelezea uamuzi wa wabunge wa Marekani kusitisha ufadhili kwa Ukraine ulioondolewa kwenye bajeti iliyopitishwa Jumamosi ili kuzuia kufungwa kwa baadhi ya shughuli za Serikali Kuu, ni kama tukio la muda tu na wala siyo kubadili kwa mfumo wa utoaji wa misaada.
Borell ambaye anaongoza mkutano wa baraza la masuala ya mambo ya nje la EU mjini Kyiv amesema anaamini kuwa suluhisho litapatikana la kuendelea kutolewa kwa msaada wa Marekani kwa Ukraine.
Forum