Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:06

Ukraine inaripoti mashambulizi mapya ya anga ya Russia dhidi ya Kyiv


Mfano wa mashambulizi ya anga yanayoendelea huko Kyiv. March 26, 2022.
Mfano wa mashambulizi ya anga yanayoendelea huko Kyiv. March 26, 2022.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba kulikuwa na milipuko sehemu za kati kati ya mji na kuwaeleza watu waendelee kubaki kwenye makazi yao

Maafisa wa Ukraine leo Jumatatu wameripoti mashambulizi mapya ya anga ya Russia dhidi ya Kyiv baada ya mashambulizi makali ya anga katika mji mkuu wa Ukraine.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba kulikuwa na milipuko sehemu za kati kati ya mji na kuwaeleza watu waendelee kubaki kwenye makazi yao. Mashambulizi hayo ya Jumatatu yalifuatia kile Klitschko alichokiita usiku mwingine mgumu kwa mji mkuu.

Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji huo, amesema vikosi vya Russia vilitumia mchanganyiko wa makombora ya masafa marefu na ndege zisizo na rubani, katika shambulio hilo la usiku kucha, na kuilenga Kyiv kwa mara ya 15 mwezi Mei.

Mashambulizi hayo ya anga yamekuja kabla ya kutarajiwa kwa Ukraine kukabiliana na mashambulizi ambayo viongozi wa Ukraine wamesema yatajaribu kuyakomboa maeneo ambayo Russia iliyateka tangu ilipoanzisha uvamizi kamili kwa Ukraine mwanzoni mwa mwaka jana.

Forum

XS
SM
MD
LG