Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:42

Uhuru Kenyatta anatoa wito wa kusitishwa mapigano mashariki mwa DRC


Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni mpatanishi katika mzozo wa eneo hilo tete kwa niaba ya nchi saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki."Alielezea wasiwasi mkubwa juu ya hali inayozidi kuzorota" huko Kivu Kaskazini ambako mapigano yamezuka "kati ya makundi mbalimbali yenye silaha

Kiongozi wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumatano ametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako matatizo yanayoongezeka yamezua mivutano ya kidiplomasia kati ya DRC na Rwanda.

Kenyatta ni mpatanishi katika mzozo wa eneo hilo tete kwa niaba ya nchi saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

"Alielezea wasiwasi mkubwa juu ya hali inayozidi kuzorota" huko Kivu Kaskazini ambako mapigano yamezuka "kati ya makundi mbalimbali yenye silaha, Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Congo (FARDC) na M23," ofisi yake ilisema katika taarifa.

Taarifa hiyo ilitolewa siku moja baada ya Rwanda kuifyatulia risasi ndege ya kivita kutoka DRC ambayo serikali mjini Kigali ilidai ndege hiyo iliingia katika anga yake.

Kinshasa imekanusha kuwa moja ya ndege zake zilikuwa zimeruka juu ya anga ya Rwanda, na kuishutumu Kigali kwa shambulio dhidi ya ndege hiyo ambayo ilisema ni sawa na "kitendo cha vita".

DRC pamoja na Marekani na nchi kadhaa za Ulaya mara kadhaa zimekuwa ziki-ishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi, madai ambayo Kigali inakanusha.

Kenyatta hakuzungumzia tukio hilo la ndege ya kivita lakini alitoa wito wa "kusitishwa kwa uhasama wa aina yoyote" na kuheshimu mazungumzo ya amani yaliyofanyika katika mji mkuu wa Angola, Luanda na Nairobi nchini Kenya ambayo yalifungua makubaliano ya kusitisha mapigano.

XS
SM
MD
LG