Mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la dunia baada ya Carlo Puyol kuweka kimiani kwa kichwa bao la pekee na la ushindi kwa timu yake katika dakika ya 73.
Mchezo huo uliotawaliwa kwa kiasi kikubwa na Hispania uliwapa nafasi mabingwa hao wa Ulaya kuendeleza ubabe kwa Ujerumani.
Fainali itachezwa Jumapili ikiwa ni fainali ya kwanza kwa Hispania na ya tatu kwa Uholanzi lakini timu zote hakuna iliyowahi kuchukua ubingwa huo.
Na mchezo wa mshindi wa tatu utakuwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.
Bingwa wa mara tatu wa kombe hili Ujerumani wamejikuta wakicheza tena mechi ya mshindi wa tatu kama ilivyokuwa mwaka 2006.