Watu wenye misimamo mkali na waasi wameongeza mashambulizi ili kuongeza utawala wao na udhibiti wa rasilimali katika jamii. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Human Rights Watch na Amnesty International wamesema Alhamisi kwamba raia wanaendelea kuuwawa, kutekwa nyara na kunyanyaswa ikiwemo nchini Burkina Faso ambako makundi ya wanajihadi yamekuwa yakipigana kwa miaka mingi, pamoja na Mali ambako wanamgambo na makundi ya kikabila ya waasi wamekuwa wakipanua ushawishi wao.
Ilaria Allegrozii ambaye ni mtafiti mashuhuri wa Human Rights Watch amesema kwamba mauaji ya raia ya Mali kutoka kwa makundi ya kiislamu pamoja na jeshi la Mali ni uhalifu wa kivita unaohitaji kuchunguzwa kwa kina. Ripoti ya Human Rights Watch iliwasilishwa kwa wizara za Sheria na Ulinzi za Mali, lakini hazijatoa majibu yoyote kufikia sasa kulingana na kundi hilo.
Forum