Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 01:10

Uchunguzi wa rushwa dhidi ya Zuma waashiria ufisadi wa kimfumo

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipohutubia wafuasi wake mbele ya nyumba yake ya kijijini huko Nkandla baada kupewa kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama. Julai 4, 2021
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipohutubia wafuasi wake mbele ya nyumba yake ya kijijini huko Nkandla baada kupewa kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama. Julai 4, 2021

Uchunguzi wa rushwa nchini Afrika Kusini uliashiria ufisadi wa kimfumo wakati wa uongozi wa Rais wa zamani Jacob Zuma katika sehemu ya kwanza ya ripoti yake iliyochapishwa Jumanne, baada ya zaidi ya miaka mitatu ya uchunguzi uliohusisha zaidi ya mashahidi 300.

Uchunguzi huo ulioongozwa na jaji mkuu Raymond Zondo ulianzishwa mwaka 2018 ili kuchunguza madai ya ufisadi wa hali ya juu wakati wa miaka tisa ya Zuma madarakani kuanzia mwaka 2009, baada ya kashfa na ulaghai kugubika siasa za Afrika Kusini kwa miaka mingi.

Zuma anakanusha kufanya makosa na amekataa kushirikiana na uchunguzi huo, na kusababisha kufungwa kwake mwezi Julai kwa kudharau mahakama. Aliachiliwa kwa msamaha wa kiafya mnamo Septemba kabla ya kuamriwa kurudi tena gerezani na mahakama kuu uamuzi ambao ameukatia rufaa.

Tuhuma zilizotolewa dhidi ya Zuma ni pamoja na kuwaruhusu wafanyabiashara wa karibu nae ambao ni ndugu Atul Ajay na Rajesh Gupta kupora rasilimali za serikali na kushawishi sera, katika kile kinachojulikana sana nchini Afrika Kusini kama kukamata serikali.

XS
SM
MD
LG