Baadhi ya wanawake ikiwa ni pamoja na mwanachama wa vyama vya wafanyakazi, mmoja wa aliyeshiriki vita vya ukombozi, mwandishi na mwanamitindo wanagombea urais nchini Zimbabwe. Na bila ya kujali kama watashinda au la wanawake hao wanaweka historia nchini humo.
Wamekuwa miongoni mwa wagombea waliovunja rekodi 22 katika kinyang’anyiro cha urais wa nchi hiyo Jumatatu Julai 30 ulio na ushindani tangu nchi hiyo kupata uhuru wake 1980 , na pia ni uchaguzi wa kwanza bila mgombea aliyekuwa kiongozi wa kiimla Robert Mugabe ambaye aliondolewa na jeshi mwezi November.
Uchaguzi huo wa rais unafikiriwa kuwa unaweza kwenda kwa yeyote kati ya rais wa sasa Emmerson Mnangangwa, mwenye umri wa miaka 75 wa chama tawala Zanu-PF party, na Nelson Chamisa, miaka 40 anayeongoza muungano wa Movement for Democratic Alliance.