Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:03

Timu za waokozi zaendelea kusaka majeruhi kutokana na mlipuko wa Ibadan, Nigeria


Timu za waokozi wa Nigeria zikibeba watu waliojeruhiwa baada ya jengo lao kuporomoka mjini Lagos. Picha ya maktaba. Reuters Machi 15. 2020
Timu za waokozi wa Nigeria zikibeba watu waliojeruhiwa baada ya jengo lao kuporomoka mjini Lagos. Picha ya maktaba. Reuters Machi 15. 2020

Timu za waokozi za Nigeria Jumanne usiku zimeendelea kuwasaka watu waliojeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa kwenye jimbo la Oyo, ambao ulitikisa majengo, na kupelekea wakazi kutorokea barabarani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, chanzo cha mlipuko huo hakijabainishwa, wakati baadhi ya vyombo vya habari vya ndani vikiripoti kwamba majengo kadhaa yaliporomoka.

Mlipuko huo unaripotiwa kusikika kwenye mji mkuu wa jimbo la Oyo wa Ibadan, uliyoko umbali wa kilomita 130 kutoka kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria wa Lagos.

Awali mkuu wa mawasiliamo wa jimbo hilo Prince Dotun Oyelade alisema kwamba wakazi wa Ibadan pamoja na vitongoji vyake, walisikia mlipuko usio wa kawaida, mida ya saa 2 za usiku. Serikali ya jimbo imeomba wakazi kuwa watulivu, wakati ikiendelea kushugulikia mkasa huo.

Forum

XS
SM
MD
LG