Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:18

Tanzania yatoa wito wa kudumishwa amani Sudan Kusini


Watu walopoteza makazi yao ndani ya kambi ya Umoja wa Matiafa huko Tomping karibu na Juba Sudan Kusini.
Watu walopoteza makazi yao ndani ya kambi ya Umoja wa Matiafa huko Tomping karibu na Juba Sudan Kusini.
Mazungumzo ya kukomesha uhasama na kusitisha mapigano huko Sudan Kusini yakiwa yanaendelea pole pole mjini Addis Ababa, Ethopia, mapigano yanaripotiwa kuendelea katika sehemu mbali mbali ya nchi hiyo.

Ghasia katika taifa hilo jipya la dunia limezusha wasi wasi mkubwa katika bara la afrika na Jumuia ya KImataifa ambapo viongozi mbali mbali wanajaribu kutumia ushawishi wao kutaka pande mbili zinazogombana kufikia makubaliano kwa njia ya majadiliano.

Tanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijaribu kusaidia katika kutanzua migogoro ya bara la Afrika imetoa wito wa kudumishwa tena amani. Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya mabo ya nje ya Tanzania Balozi Vincent KIbwana anasema "Tanzania ingelipenda kuona nchi hiyo inarudi katika hali ya usalama, amani na umoja kwa haraka iwezekanavyo"

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Balozi Kibwana anasema kutokana na kwamba Tanzania ni mwanachama moja wapo ya mataifa 15 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, inachangia katika juhudi za kudumisha amani barani Afrika, na anasema,

"Kwa kweli Tanzania na nchi zote wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la AU wanajipanga kuona kwamba mwaka 2014 tunamaliza migogoro inayoendelea na tunajipanga zaidi kuzuia migogoro mipya."

Anasema hiyo ndiyo maana baraza hilo linasisitiza juu ya haja ya kuundwa jeshi la pamoja
la Umoja wa Afrika "African Standby Force" ili liweze kushughulikia matatizo kama hayo mapema kabla hayajasamba zaidi. .
XS
SM
MD
LG