Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 04:02

Wawakilishi wa Upinzani Zanzibar Wapinga Kurudiwa Uchaguzi


Vijana wafuasi wa CUF wakicheza na kushangilia wakitabiri ushindi wa wagombea wao.
Vijana wafuasi wa CUF wakicheza na kushangilia wakitabiri ushindi wa wagombea wao.

Hali ya kisiasa visiwani Zanzibar baada ya kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu bado ni tete huku kila kundi likija na matamko ya kukinzana juu ya hatma ya siasa za visiwa hivyo vinavyounda jamhuri ya muungano wa Tanzania.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jijini Dar es salaam wagombea 27 wa Baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF wanaodai wameshinda kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, wamesema hawapo tayari kurudia zoezi la uchaguzi mkuu kama tume ya Uchaguzi Zanzibar ilivyotangaza wakati Mwenyeketi wa Tume hiyo Jecha Salim Jecha alipotangaza kufuta uchaguzi kwa madai haukuwa huru na haki.

XS
SM
MD
LG