Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 01:06

Rais mpya Tanzania afuta safari za nje


Rais wa Tanzania John Magufuli baada ya kuapishwa
Rais wa Tanzania John Magufuli baada ya kuapishwa

Rais mpya wa Tanzania John Magufuli amepiga marufuku safari za nje ya nchi kwa maafisa wa serikali hiyo ila tu itakapokuwa lazima na kwa ruhusa ya ikulu.

Katika mkutano wake wa kwanza na watendaji wa serikalini kama vile makatibu wakuu wa wizara na maafisa wanaoongoza taasisi muhimu Rais Magufuli alisema shughuli nyingi za nje ya nchi zitafanywa na kusimamiwa na mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi hizo.

Rais huyo ambaye alichukua madaraka Novemba 5 aliwataka maafisa wa serikali badala yake wafanye zaidi ziara za vijijini ili kufahamu shida zinazowakabili wananchi vijijini.

Amri hiyo inaonekana kuwa tofauti sana na utawala uliopita wa Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akilalamikiwa sana nchini humo kwa kufanya safari nyingi za nje ya nchi.

Rais Magufuli alitangaza kuwa kuanzia Januari 2016 wanafunzi wote ambao watakuwa wanaanza shule hawatalipa ada. Kimsingi shule za msingi Tanzania hazina ada lakini wanafunzi wamekuwa wakilipa michango kadha ambayo ilikuwa inaonekana kama ada.

XS
SM
MD
LG