Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Tanzania vyama vya siasa nchini humo vimekuwa vikitumia kauli mbiu mbali mbali ambazo zinaashiria sera zao na namna ya kuwatia hamasa wafuasi wao au kuvutia wafuasi wapya.
Kauli mbili hizo zimekuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya kampeni mwaka huu, na kufanya kampeni hizo kuwa tofauti kabisa na ilivyokuwa katika miaka ya iliyopita.
Miongoni mwa mambo yalipamba kampeni za mwaka huu ni pamoja na wasanii, viongozi wa dini kushiriki kwa kiasi kikubwa katika kampeni. Kauli za kila aina nazo zimekuwa kivutio ndani ya vyama hivi.