Kundi la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights limesema kwamba takriban watu 75 walishambuliwa na kundi hilo Jumamosi kwenye eneo la mashambani la Homs mashariki mwa taifa hilo.
Watu 10 waliuwawa akiwemo mwanamke mmoja, pamoja na mpiganaji kutoka vikosi vya utawala wa Syria, huku baadhi ya watu wakiwa hawajulikani walipo, ripoti ya kundi hilo imeongeza.
Shirika la habari la serikali ya Syria la SANA limeripoti kuhusu shambulizi hilo ingawa limetoa idadi ndogo ya waliokufa ikilinganishwa na ripoti ya awali.
Ghasia za Syria zilizoanzishwa na harakati za kukomesha maandamano ya kudai demokrasia miaka kadhaa iliyopita, zimeua takriban watu nusu milioni kufikia sasa, huku takriban nusu ya wakazi wa taifa hilo wakilazimika kuondoka makwao.