Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 04:46

Marekani: Taarifa za mitandao ya kijamii ya Waomba Viza kuchunguzwa


Viza ya kuingia Marekani.
Viza ya kuingia Marekani.

Serikali ya Marekani imetangaza kwamba maafisa wa uhamiaji sasa wanahitajika kuchunguza taarifa za mitandao ya kijamii ya watu wanaoomba kibali (viza) cha kuingiza nchini.

Kanuni hizo mpya, ambazo madhumuni yake makubwa ni kukabiliana na ugaidi na chuki, pia zinawaagiza watu wote ambao wanafanya maombi ya viza za kutembea Marekani kuorodhesha anwani zao za barua pepe na nambari za simu ambazo wamekuwa wakitumia kwa angalau miaka mitano kabla ya kutuma maombi hayo.

Hata hivyo, baadhi ya watu ambao wana vyeti vya kusafiria vya kidiplomasia, huenda wasihitajike kutimiza masharti hayo.

Kanuni hizo zilipendekezwa mwaka jana kwa mara ya kwanza.

Maafisa wa serikali ya Marekani wanasema kuwa wanaoomba viza, pia wataulizwa iwapo wamewahi kushiriki katika vitendo vya kigaidi.

Kwa mujibu wa idara husika, maagizo hayo yataathiri takriban wageni milioni 15 kutoka nchi za nje.

Tangu Rais Donald Trump kuingia madarakani, utawala wake umechukua hatua mbalimbali katika juhudi za kukabiliana na uhamiaji haramu.

XS
SM
MD
LG