Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:53

Uswiss yaishangaza Spain 1-0


Uswiss imeshangaza fainali za Kombe la Dunia Jumatano kwa ushindi usiotazamiwa dhidi ya Spain

Timu ya taifa ya Uswiss imeushangaza ulimwengu wa soka Jumatano baada ya kuifunga Spain 1-0 katika mechi ya kundi H mjini Durban. Gelson Fernandes alipata bao la Uswiss katika dakika ya 52, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Uswiss kuifunga Spain katika mechi 19.

Spain timu inayoshikilia nafasi ya pili katika orodha ya timu bora ya FIFA duniani ilitazamiwa kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa ushindi dhidi ya Uswiss, na kwa muda mrefu walitawala mchezo lakini ulinzi mkali wa Uswiss ulifanya iwe vigumu kwa Spain kupata goli. Mpaka halftime hakuna aliyekuwa amepata goli.

Lakini dakika chache baada ya kurudi kwa kipindi cha pili Fernandes akafunga goli ambalo huenda likasikika kote katika ulimwengu wa kandanda. Spain watapata nafasi nyingine Jumatatu ijayo watakapopambana na Honduras mjini Johannesburg.

Katika mechi ya awali Chile iliifunga Honduras 1-0 na kuanza vizuri fainali hizo kwa goli lililofungwa na Jean Beausejour katika dakika ya 34.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG