Baada ya miaka kadhaa ya shinikizo la kimataifa Sudan Kusini inasema inapanga kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari Christopher Allen aliyeuawa mwaka 2017 wakati akiripoti vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha umwagaji damu nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Martin Elia Lomuro alitangaza katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni kwamba kamati imeundwa ili kuchunguza mazingira ya kifo cha mwandishi wa habari Christopher Allen.
Marekani na Uingereza pamoja na makundi ya kampeni za vyombo vya habari na familia ya Allen, kwa muda mrefu wametaka uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji yake yaliyotokea Agosti 26, mwaka 2017.
Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 26, mwenye uraia wa nchi mbili Marekani na Uingereza, alipigwa risasi kichwani wakati wa mapigano kati ya jeshi la Sudan Kusini na waasi katika mji wa kusini magharibi wa Kawa.
Forum