Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:22

Spika wa bunge la Somalia  alaani vikali shambulio kwenye kambi ya jeshi


Wanajeshi wa Somalia wakiwa kwenye kambi ya jeshi la Somalia, karibu na eneo la shambulizi la al-Shabab.(AP)
Wanajeshi wa Somalia wakiwa kwenye kambi ya jeshi la Somalia, karibu na eneo la shambulizi la al-Shabab.(AP)

Spika wa bunge la Somalia  amelaani vikali shambulio la Jumatatu la woga lisilo na huruma na lisilo na utu au kumuogopa Mungu katika kambi ya kijeshi lililouwa wanajeshi 25 na kujeruhi wengine zaidi ya 70.


Sheik Adan Mohamed Nur, maarufu kama Adan Madobe, amesema anashuku wasaliti wanaweza kuwa walifanikisha shambulio hilo la bomu.

Najua kati ya maafisa wa Polisi wako ambao ni wazuri, wachapa kazi na wenye heshima lakini wasaliti wamewezesha hili. Ninashuku hilo sana. Haivumiliki alisema kwenye video iliyowekwa na vyombo vya habari vya serikali.


Kundi la wanamgambo wa al-Shabab lilidai kuhusika na shambulio hilo. Katika taarifa kwenye mtandao wa Telegram, al-Shabab ilisema mmoja wa washambuliaji wake wa kujitoa muhanga ndiye aliyetekeleza shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG