Mwezi uliopita, shilingi ya Uganda ilishuka kwa kiwango cha chini mno. Wachuuzi ambao wanalipa kodi yao kwa dola ya Marekani wameona kupanda kwa kiasi kikubwa kwa gharama, huku baadhi ya vituo vya afya vikiwa vimeanza kutoza gharama kwa dola badala ya shilingi.
Kuna vigezo kadhaa ambavyo vimesababisha shilingi kuanguka, ikiwemo uchumi wenye nguvu wa Marekani na kushuka kwa mauzo ya nje ya mazao kwa nchi iliyokumbwa na mzozo ya Sudan Kusini.
Mkurugenzi wa utafiti katika benki ya Uganda, James Opolot anasema kushuka kwa bei za bidhaa pia kumechangia katika maumivu hayo hasa kwa vile nchi inauza nje bidhaa zilizotengenezwa.
Ingawaje shilingi imebakia kuwa chini, kuna uthabiti uliopatikana kutokana na uingiliaji kati kutoka benki ya Uganda. Maafisa wengi wanalaumu kushuka huko kwa kasi kunatokana na habari za kusisimua katika vyombo vya habari ambazo zimesema kuwa benki huenda haitaingilia kati tena katika soko la fedha.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa benki ya Uganda, Christine Alupo anasema hilo si kweli, lakini ameongezea kuwa banki haitaki na wala haiwezi kuingilia kati kila wakati.
“Huo umekuwa ni ujumbe wetu wakati wote. Ujumbe wetu siku zote umekuwa kwamba uingiliaji kati wetu uko ndani ya misingi inayokubali kama kuna hali tete sana na hivyo tunajaribu kurejesha uthabiti kwenye soko na tumeiangalia hali kulingana na vigezo ambavyo si vya msingi sana,” amesema Bi Opolot.
Lakini kudhoofika kwa shilingi kumefanya hali kuwa ngumu kwa wafanyakazi wa kigeni. Jenney Smith anasema akiwa na familia ya kuihudumia hili linafadhaisha sana.
“Kwa kweli, mshahara wangu kihalisia umeshuka kwa dola 100 kwa mwezi, hivyo ndivyo ilivyo. Na bei za kila kitu zimepanda hivi karibuni, bei kwenye maduka ya vyakula ziko juu. Si kwa kiwango kikubwa lakini zimepanda. Kwahiyo ukichanganya na fedha kidogo na halafu gharama nyingine zilizo juu, huwezi kukidhi mahitaji kama ilivyokuwa hapo kabla. Nahisi kama hali itakuwa mbaya zaidi wakati tukikaribia uchaguzi,” amesema Bi Smith.
Ingawaje wengi wanalaumu uchaguzi ujao kwa hali hii ya kushuka kwa htamani ya shilingi, maafisa wa benki wanasema kama watu watakuwa watulivu na kuendelea kuwekeza kama kawaida, hali itakuwa thabiti hapo baadaye.
Lakini kwa wale ambao wanapambana na maisha kutokana na hali ya sasa wanasema muda unayoyoma.