Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 20:52

Shambulizi la bomu lauwa watatu Mogadishu


Afisa wa polis akiangalia mabaki ya gari lilikuwa na bomu , April, 21, 2014.
Afisa wa polis akiangalia mabaki ya gari lilikuwa na bomu , April, 21, 2014.

Shambulizi la bomu ndani ya gari limeshambulia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kuuwa takriban watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa.

Shambulizi la Jumatano limefanyika karibu na mji wenye ulinzi mkali ulioko uwanja wa ndege wa kimataifa ambao una nyumba na maofisi ya balozi za kigeni na kituo cha umoja wa mataifa.

Msemaji wa umoja wa mataifa amesema wafanyakazi wa umoja wa mataifa walijeruhiwa au kuuwawa kwenye mlipuko huo.

Kundi la wanamgambo la Al- shaabab limedai kuhusika na kusema katika taarifa yake kwamba wapiganaji wake walilenga ujumbe wa kigeni na washirika wake.

Al- shaabab imepoteza nguvu nchini Somalia dhidi ya jeshi la umoja wa Afrika lakini limefanya mashambulizi kadhaa huko Mogadishu katika miaka ya hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG