Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 03:41

Tanzania yasisitiza kupambana na wasio waadilifu


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea moja ya kambi za wakimbizi nchini humo.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea moja ya kambi za wakimbizi nchini humo.

Serikali ya Tanzania imesisitiza kwamba itaendelea kupambana na watumishi wa umma wasio waadilifu na wala rushwa licha ya kuwepo malalamiko kwamba kuna baadhi ya watumishi wa umma nchini humo ambao kwa sasa wanaishi kwa hofu ya kupoteza kazi zao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hofu hiyo ya kupoteza kazi kwa baadhi ya watumishi wa umma nchini Tanzania imetokana na kasi ya uwajibishwaji kwa watumishi wanaodaiwa kukiuka maadili na misingi ya kazi katika maeneo husika na kupewa jina maarufu la “utumbuaji wa majipu”.
kauli hiyo ya serikali ilitolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipozungumza na mawaziri na manaibu mawaziri wote wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mafunzo kuhusu mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa ahadi ya uadilifu, iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa


Waziri Mkuu alisema mtumishi yeyote wa umma anayeishi kwa hofu ya kuwajibishwa ni yule aliye mchafu, na serikali itaendelea kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume na maadili ya uongozi

Awali Kamisha wa maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda alimweleza Waziri Mkuu kwamba atamkabidhi majina ya baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri ambao mpaka sasa hawajajaza fomu ya maaadili.
Tayari watumishi kadhaa wa sekta mbalimbali za umma nchini Tanzania wamesimamishwa kazi na wengine kuchukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma za ubadhirifu katika sehemu zao za kazi tangu kuingia madarakani kwa Rais John Magufuli.

XS
SM
MD
LG