Katika barua kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Seneta Robert Menendez alitoa wito wa tathmini ya kina ya sera ya Marekani kwa Rwanda.
Menendez alisema ataanza kwa kusimamisha dola milioni kadhaa kuwasaidia walinda amani wa Rwanda wanaoshiriki katika shughuli za Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa barua hiyo, ambayo ilivujishwa kwenye vyombo vya habari na ambayo ofisi yake ilithibitisha kuwa ni ya kweli. Hatua hiyo iliyochukuliwa ni utaratibu wa Seneti unaozuia hoja kufika kwenye ngazi ya kupiga kura.
Menendez alisema anahofia kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa jeshi la Rwanda wakati linatumwa Congo na kuwaunga mkono waasi utatoa ishara ya kutatanisha kwamba Marekani inaidhinisha kimya kimya vitendo hivyo.