Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:32

Jinsi Senegal ilivyokosa kuingia raundi ya pili


Yerry Mina aifungia Colombia goli la ushindi dhidi ya Senegal.
Yerry Mina aifungia Colombia goli la ushindi dhidi ya Senegal.

Huenda ukajiuliza imekuwaje Senegal imetolewa katika fainali za kombe la dunia wakati imefungana sawa na Japan katika pointi, magoli ya kufunga na kufungwa?

Jibu ni kwamba: Senegal imetolewa katika mashindano hayo kwa sheria inayoitwa "fair play" - yaani uchezaji unaozingatia kanuni. Baada ya kufungwa 1-0 na Colombia Alhamisi Senegal imemaliza katika Kundi H ikiwa imefungana kwa kila kitu na Japan.

Timu zote mbili zimemaliza zikiwa na pointi 4 kila moja, kila moja imefunga magoli manne na kufungwa magoli manne. Mpaka hapo timu hizo zimefungana katika kila eneo. Baada ya hapo iliangaliwa je timu hizo zilipokutana matokeo yalikuwaje. Hapo pia zilifungana kwa sababu zilitoka sare 2-2.

Katika hali hiyo sheria za FIFA zinakwenda hatua ya sita ambayo inaweza kutenganisha timu hizo. Na hapo ndipo sheria ya "fair play" inapozingatiwa - yaani timu gani imepata kadi chache za njano au nyekundu.

Senegal ilikuwa imepata kadi za njano sita katika mechi zote tatu. Japan ilipata kandi nne tu za njano. Hiyo ndio iliyoivusha Japan kuingia raundi ya pili, na Senegal kurudi nyumbani.

XS
SM
MD
LG