Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:34

Saudi Arabia inataka kushirikiana na sio kushindana na China;Abdulaziz bin Salman


Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman wa Saudi Arabia
Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman wa Saudi Arabia

Ushirikiano kati ya Riyadh na Beijing pia umeimarishwa katika usalama na teknolojia nyeti huku kukiwa na ongezeko la uhusiano wa kisiasa unaotiliwa wasiwasi na Marekani

Saudi Arabia inataka kushirikiana na sio kushindana na China, waziri wa nishati katika ufalme wa Saudi Arabia alitangaza Jumapili akisema alipuuzia wasiwasi wa Magharibi juu ya uhusiano wao unaokua. Kama muuzaji mkuu wa mafuta duniani uhusiano wa Saudi Arabia na watumiaji wakubwa wa nishati duniani unaangaziwa na uhusiano wa hydrocarbon.

Lakini ushirikiano kati ya Riyadh na Beijing pia umeimarishwa katika usalama na teknolojia nyeti huku kukiwa na ongezeko la uhusiano wa kisiasa unaotiliwa wasiwasi na Marekani. Alipoulizwa kuhusu ukosoaji wa uhusiano wa nchi mbili wakati wa mkutano wa kibiashara kati ya nchi za Kiarabu na China, mwana mfalme Abdulaziz bin Salman alisema na hapa ninamnukuu, Kwa kweli ninalipuuzia hilo kwa sababu Kama mfanya biashara, hivi Sasa utaelekea mahali ambapo fursa inakuja kwenye njia yako.

Hatuna haja ya kuwa na chaguo lolote ambalo linahusiana na kusema, ama sisi au na wengine, alisema mwana mfalme. Wajasiriamali na wawekezaji wa China wanajumuika Riyadh kwa ajili ya mkutano huo ambao umekuja siku chache baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Forum

XS
SM
MD
LG