Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:53

Saudi Arabia imepeleka dola bilioni 2 kwa benki kuu ya Pakistan


Waziri wa fedha wa Pakistan, Ishaq Dar
Waziri wa fedha wa Pakistan, Ishaq Dar

Waziri wa Fedha wa Pakistan Ishaq Dar alisema ufalme wa Saudi Arabia unafanya vyema katika ahadi yake ya kuimarisha akiba ya fedha za kigeni za Pakistan. Utaratibu huu sio mkopo lakini utaongeza akiba kuendelea kuwepo katika benki kuu ya Pakistan kwa angalau mwaka mmoja

Saudi Arabia imepeleka dola bilioni 2 katika benki kuu ya Pakistan, serikali imesema Jumanne, hatua ya kifedha inayohitajika sana kabla ya mkutano muhimu wa shirika la fedha duniani (IMF) kuhusu mpango mpya wa fedha za uokoaji kwa nchi hiyo ya kusini mwa Asia.

Katika taarifa kwa njia ya video, Waziri wa Fedha wa Pakistan Ishaq Dar, alisema ufalme huo unafanya vyema katika ahadi yake ya kuimarisha akiba ya fedha za kigeni za Pakistan. Utaratibu huu sio mkopo lakini utaongeza akiba kuendelea kuwepo katika benki kuu ya Pakistan kwa angalau mwaka mmoja.

Hatua hiyo inakuja wakati wa mkutano wa bodi ya utendaji ya IMF ambayo inatarajiwa kuidhinisha mkopo mpya wa dola bilioni 3 kwa Pakistan ili kuisaidia nchi hiyo kuondokana na mgogoro wa kiuchumi.

Dar alisema kwa amana ya Saudi Arabia akiba ya fedha za kigeni ya Pakistan ambayo imeshuka hadi dola bilioni 9.6 wiki iliyopita, haitoshi kulipa bili zinazoingia kwa mwezi, ambazo zimepanda hadi dola 11.6 bilioni.

Forum

XS
SM
MD
LG