Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 19:23

Russia kusitisha huduma za mamluki wa Wagner hivi karibuni


Picha inayojumuisha wanajeshi wa Belarus na mamluki wa Wagner.
Picha inayojumuisha wanajeshi wa Belarus na mamluki wa Wagner.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Ijumaa kwamba kundi la mwisho la mamluki wa Wagner ambao ni wafungwa walioachiliwa, na wanaotumikia serikali litasitisha huduma zake hivi karibuni.

Kwenye ripoti ya kiintelijensia ya kila siku kutoka wizara hiyo huhusiana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, wizara hiyo imesema kwamba wafungwa kadhaa waliosamehewa wataendelea kuhudumu kama mawakala kwenye kundi la Wagner, na kwamba Russia sasa hivi inadhibiti mfumo wa kuwatumia wafungwa hao.

Kundi la Wagner mwezi uliopita lilifanya jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa Rais Vladimir Putin. Kusitishwa kwa program ya kutumia wafungwa kutoka kundi hilo kutafikisha kikomo moja wapo ya vipindi hatari zaidi katika historia ya kijeshi nchini Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kwamba hadi mamluki 20,000 wameuwawa ndani ya miezi michache iliyopita. Mkuu wa idara ya CIA William Burns amesema Alhamisi kwenye kikao cha Usalama cha Aspen cha kitaifa hapa Marekani kwamba huenda Putin anavuta muda kabla ya kulipiza kisasi dhidi ya kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin kutokana na jaribio hilo la mapinduzi.

Forum

XS
SM
MD
LG