Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:00

Ronaldo atisha Kombe la Dunia 2018


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo, akishangilia moja ya magoli yake, Ijumaa.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo, akishangilia moja ya magoli yake, Ijumaa.

Christiano Ronaldo amedhihirisha ubora wake baada ya kuifungia timu yake ya Ureno, magoli matatu na kufanikiwa kujiepusha na kipigo kutoka kwa Uhispania, mjini Sochi, nchini Russia, Ijumaa.

Mchezaji huyo anayeshikilia taji la mchezaji bora wa dunia kwa mwaka huu 2018, alianza kuifungia Ureno goli la kuongoza katika dakika ya nne kwa njia ya penati na kufunga tena dakika za 44, na 88.

Nahodha wa Ureno Christiano Ronaldo, (kushoto) na Sergio Ramos (kulia) wakiwa na waamuzi kabla ya mchezo mjini Sochi, Russia, Ijumaa.
Nahodha wa Ureno Christiano Ronaldo, (kushoto) na Sergio Ramos (kulia) wakiwa na waamuzi kabla ya mchezo mjini Sochi, Russia, Ijumaa.

Uhispania ambayo ilipatwa na mshangao wa kufukuzwa kwa kocha wake Julen Lopetegui siku mbili kabla ya mashindano kuanza baada ya kutangazwa kuifungisha Real Madrid, msimu ujao, ilionyesha kiwango kizuri cha mchezo lakini firimbi ya mwisho ilipolia Christiano Ronaldo alitoka kifua mbele.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ureno
Kikosi cha timu ya taifa ya Ureno

Fernando Hierro, kocha wa Uhispania wa sasa alishuhudia timu yake ikirudisha magoli baada ya kuwa nyuma mara mbili ambapo Diego Costa alifunga magoli mawili ya kusawazisha, kabla ya kuongoza mpaka dakika ya 88 Ronaldo alipofunga.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania.
Kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania.

Kutokana na matokeo haya, timu ya Iran inaongoza kundi B kwa pointi tatu kwa kuifunga Morocco (1-0) iliyopoteza mchezo katika mazingira kama ya Misri. Uhispania na Ureno zenyewe zipo nafasi ya pili na tatu kwa kuwa na pointi moja kila moja.

XS
SM
MD
LG