Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 12:22

Ripoti zinatofautiana juu ya wanaharakati 290 waliokamatwa Islamabad


Maandamano ya wanaharakati wa Baloch Solidarity Committee nchini Pakistan
Maandamano ya wanaharakati wa Baloch Solidarity Committee nchini Pakistan

Baloch Solidarity Committee iliiambia VOA, Idhaa ya ki-Urdu kwamba zaidi ya waandamanaji 160 wameachiliwa lakini zaidi ya 100 bado wako chini ya ulinzi wa polisi.

Maafisa wa serikali nchini Pakistan wanadai kuwa wamewaachia huru wanaharakati 290 waliokamatwa mjini Islamabad, wakati kundi la wanaharakati hao baadaye limesema zaidi ya watu 100 bado wako jela, huku baadhi yao wakiwa hawajulikani walipo.

“Maandamano ya amani ni haki ya kila mtu, lakini hakuna anayeweza kuchukua sheria mikononi mwake”, ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, wakati ikitangaza kuachiliwa kwa wanaharakati wa Baloch.

Baadaye, Baloch Solidarity Committee iliiambia VOA, Idhaa ya ki-Urdu kwamba zaidi ya waandamanaji 160 wameachiliwa, lakini zaidi ya 100 bado wako chini ya ulinzi wa polisi “na baadhi yao hawajulikani walipo”, na kwamba polisi wa Islamabad “hawakutoa taarifa sahihi kwao pamoja na vyombo vya habari”.

Wanaharakati wa Baloch walisafiri kuelekea mji mkuu kwa msafara wa kupinga madai ya mauaji ya kiholela, na kulazimishwa kupotea kwa asili zao katika jimbo la kusini magharibi la Baluchistan.

Forum

XS
SM
MD
LG