Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 12:31

Ripoti ya Mo Ibrahim inasema sehemu kubwa ya Afrika sio salama


Mo Ibrahim, mwanzilishi wa taasisi ya Mo Ibrahim inayoangazia utawala bora barani Afrika
Mo Ibrahim, mwanzilishi wa taasisi ya Mo Ibrahim inayoangazia utawala bora barani Afrika

Ripoti ya taasisi yake iliyataja mapinduzi nane yaliyofanikiwa tangu mwaka 2019. Mali na nchi jirani ya Burkina Faso zimeshuhudia mawili kila moja katika kipindi hicho na kuyumbisha zaidi sehemu ya dunia ambayo tayari imezingirwa na wanamgambo wa Kiislamu

Ripoti mpya kuhusu utawala barani Afrika iliyotolewa Jumatano inabainisha sehemu kubwa ya bara hilo "ina usalama mdogo, ulinzi na demokrasia" kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita, ikitaja kuongezeka kwa mapinduzi ya kijeshi na mizozo ya silaha.

Kurudi nyuma kwa demokrasia sasa kunatishia kubadili miongo kadhaa ya maendeleo yaliyopatikana barani Afrika, kulingana na kipimo cha utawala kilichoandaliwa na taasisi ya Mo Ibrahim ambayo inaelezea mafanikio 23 na majaribio ya mapinduzi tangu 2012.

"Hali hii ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yalikuwa ya kawaida katika miaka ya 80 inaonekana tena kuwa ya mtindo katika baadhi ya maeneo ya Afrika," alisema Ibrahim, bilionea wa Uingereza aliyezaliwa Sudan ambaye anatumia utajiri wake kuhamasisha demokrasia na uwajibikaji wa kisiasa barani Afrika.

Ripoti ya taasisi yake iliyataja mapinduzi nane yaliyofanikiwa tangu mwaka 2019. Mali na nchi jirani ya Burkina Faso zimeshuhudia mawili kila moja katika kipindi hicho, na kuyumbisha zaidi sehemu ya dunia ambayo tayari imezingirwa na wanamgambo wa Kiislamu.

Waandishi wa ripoti hiyo pia waligundua matatizo ya jumla ya usalama yameenea, Katika muongo mmoja uliopita, karibu asilimia 70 ya Waafrika waliona usalama na utawala wa sheria ukipungua katika nchi zao, walisema. Zaidi ya nchi 30 zilipungua katika kitengo hiki, kulingana na kipimo hicho.

Sudan Kusini ilishika nafasi ya chini ikifuatiwa na Somalia, Eritrea, Congo, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cameroon, Burundi, Libya na Equatorial Guinea.

XS
SM
MD
LG