Wakati wa ziara hiyoTillerson ameelezea msimamo thabiti wa Marekani juu ya kushirikiana na bara hilo katika kupambana na ugaidi, maendeleo na utawala bora.
Lakini ghafla Jumanne tillerson saa chache baada ya kurejea kutoka katika ziara yake ya Afrika alifukuzwa kazi na Rais Donald Trump kama waziri wa mambo ya nje.
John Campbell ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Nigeria kuanzia mwaka 2004 hadi 2007 amesema hafahamu waafrika watachukuliaje hatua hiyo.
Campbell amesema Trump kumfukuza kazi mwanadiplomasia wa juu huenda kukatafsiria kama mfano mwingine wa utawala wake kutoliheshimu bara la Afrika na kuongeza hasa baada ya waziri huyo wa zamani kutoa uhakikisho kwenye mikutano yake.
Katika ziara yake barani Afrika Tillerson alikwenda Chad, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Nigeria.