Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 17:42

Rajoelina aelekea kushinda mhula wa tatu wa urais wa Madagascar


Rais wa Marekani Andry Rajoelina
Rais wa Marekani Andry Rajoelina

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameongeza nguvu katika uongozi wake  kwenye uchaguzi ulioshirikisha idadi ndogo ya wapiga kura na kususiwa na upinzani.

Rajoelina anaelekea kushinda muhula wa tatu Jumatatu, huku zaidi ya theluthi 3 ya vituo vya kupigia kura vikiwa vimewasilisha matokeo yao. Kiongozi huyo ambaye ni mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 49, na aliyewahi kuwa DJ, alichukua ushindi wa kisiwa hicho cha bahari Hindi kwa mara ya kwanza hapo 2009, kufuatia mapinduzi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kufikia Jumapili jioni, alikuwa tayari amepata asilimia 62.9 ya kura kutoka katika asilimia 43.1 ya wapiga kura waliojitokeza, kulingana na tume ya uchaguzi.

Waandamanaji wa upinzani walikabiliana na polisi mara kadhaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, wakidai kuwa Rajoelina hafai kuwania urais kwa kuwa alipata uraia wa Ufaransa hapo 2014, hatua wanayodai ilimuondolea uraia wake wa Madagascar na kuweka mazingira ya uchaguzi yasiyofaa. Wagombea wakuu wa upinzani wakiwemo wawili waliowahi kuwa marais walidai kuwa Rajoelina hakufaa kugombea, wakati wakiomba wafuasi wao kususia zoezi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG