Hii ni mara ya tatu kwa Mahama kuwania nafasi hiyo ya juu nchini Ghana, mojawapo ya nchi zenye demokrasia imara zaidi barani Afrika. Alishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Nana Akufo-Addo mwaka 2016 na 2020.
Uchaguzi ujao wa urais unatarajiwa kuwa na ushindani mkali. Hakuna chama ambacho kimewahi kushinda zaidi ya mihula miwili mfululizo na nchi hiyo iko katika hali mzozo mbaya wa kiuchumi katika kizazi hiki, ambao umeongeza gharama ya maisha na kusababisha sarafu ya cedi kuporomoka, na hivyo kuchochea maandamano.
Mahama, mwenye umri wa miaka 64, alipata kura 297,603, ikiwa ni asilimia 98.9 ya kura zilizopigwa, tume ya uchaguzi ilisema mapema Jumapili.