Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:00

Rais mpya wa Somalia anusurika shambulizi la bomu


Mripuko wa bomu nje ya Hoteli Jazeera Palace
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:32 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Miripuko miwili ya bomu imetikisa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Jumatano nje ya hoteli ya Al Jazeera ambako rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Sam Ongeri walikuwa wanakutana na waandishi habari.

Rais Mohamud na waziri Ongeri hawakujeruhiwa. Inaripotiwa kulikuwepo na ujumbe mkubwa wa Wakenya wakiwemo wabunge walofuatana na waziri Ongeri pamoja na wajumbe wa mashirika ya kimataifa mjini Mogadishu Waziri mkuu wa Somalia aneondoka Abdiweli Mo0hamed Ali alikua pia ndani ya hoteli wakati wa shambulio hilo.

Mwandishi wa sauti ya Amerika mjini Mogadishu anaripoti kwamba mwili wa mjitoa mhanga mmoja ulikuwa nje ya mlango wa hoteli na mwili wa mjitoa mhanga mwengine ulikuwa karibu na hoteli ndani ya gari

Takriban watu watano wameuwawa wakiwemo wanajeshi wa AMISOMO walokuwa wanalinda hoteli hiyo, na inasemekana huwenda idadi hiyo ikaongezeka.
XS
SM
MD
LG