Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 17:26

Rais wa Iran Ebrahim Raisi anaanza ziara Venezuela, Cuba na Nicaragua


Rais wa Iran, Ebrahim Raisi
Rais wa Iran, Ebrahim Raisi

Iran na Venezuela zote ni wazalishaji wakuu  wa mafuta katika Jumia ya mataifa yanayosafirisha mafuta kwa wingi duniani  OPEC na kuziweka katikati ya majadiliano ya kimataifa juu ya mgogoro wa nishati uliosababishwa na uvamizi wa Russia nchini Ukraine mwaka jana

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimeripoti Jumatano kwamba Rais Ebrahim Raisi anatarajiwa kuanza ziara ya Venezuela, Cuba na Nicaragua mwishoni mwa wiki hii.

Ziara ya Raisi, katika nchi hizo rafiki inaanza Jumapili na inalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kisayansi na mataifa matatu ya Amerika Kusini yaliyowekewa vikwazo na Marekani, shirika la habari la IRNA limesema.

Iran na Venezuela zote ni wazalishaji wakuu wa mafuta katika Jumia ya mataifa yanayosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC na kuziweka katikati ya majadiliano ya kimataifa juu ya mgogoro wa nishati uliosababishwa na uvamizi wa Russia nchini Ukraine mwaka jana.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alizuru Iran mwezi Juni 2022, akisaini mkataba wa miaka 20 wa kufungua maeneo makubwa ya ushirikiano katika sekta za mafuta, kemikali za mafuta na ulinzi. Mwezi Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian alielezea ushirikiano kati ya nchi hizo wakati alipotembelea Caracas.

Marekani tangu wakati huo imelegeza vikwazo vyake dhidi ya mafuta ghafi ya Venezuela, wakati Ufaransa imetoa wito wa kuruhusu vyanzo mbalimbali vya nishati, ikiwemo kutoka Caracas.

Forum

XS
SM
MD
LG